SIRI SABA(7) ZA KUWA HAI LEO

Habari za leo Rafiki Yangu ! .

Ningependa kukushukuru kwa wewe kuchukua muda wako na kusoma Makala mbalimbali ninazotuma kwenye page yako ya whatsapp karibia kila siku.

Leo nina zawadi nzuri kwa ajili yako uliyoisubiria sana kwa muda mrefu.  Siri 7 za Kuwa Hai Leo tayari unaweza kuzipata popote ulipo Africa Mashariki , kupitia group langu la *NDOTO NA MAFANIKIO *

Watu wengi wanajiuliza kwanini Siri 7 Za Kuwa Hai Leo? Kwanza napenda kuwajibu kwa kuwauliza Swali moja Ni nani ajuae Kesho yake? Ni nani ajuae Siku ataondoka hapa duniani? Kwa jibu rahisi ni hakuna mwenye majibu. Hivyo kama hakuna mwenye majibu kila mmoja anatakiwa ajue ni namna gani anatakiwa kuishi Leo ili endapo itatokea kesho umeondoka hapa duniani uwe kuna kitu umeacha kama alama.

Ukweli watu wengi wamepoteza maana ya Maisha wengi wanafikiri Maisha ni kuwa na mwenzi mzuri, kujenga nyumba nzuri, kuzaa watoto na kuishi Maisha mazuri. Maisha ni Zaidi yah apo rafiki yangu. Unaweza kutimiza Lengo la kuoa mke au kuolewa na mume mzuri sana lakini ukafariki wewe kabla hata hujafurahia kumpata. Unaweza kutimiza lengo la kujenga nyumba nzuri sana na ya kisasa lakini ukafariki kabla hujaishi humo. Swali linakuja ni kitu gani kitaendelea baada ya wewe kuondoka duniani?

Umeacha mke/mume mzuri sana ataolewa/kuoa na mwingine. Umeacha nyumba nzuri watakuja kugawana ndugu zako au uliowaachia urithi. Je dunia itafaidika nini kwa uwepo wako hapa duniani? Hapo utakuta hakuna itakachofaidi.

Sasa *ndugu *nataka unielewe vizuri sijasema usioe au kuolewa, sijasema usijenge nyumba nzuri sijasema usiweke lengo la kuwa na gari au watoto. Maana yangu hapa ni hayo yasiwe malengo makuu ya Maisha yako. Kwanini yasiwe malengo makuu? Kwasababu unaweza kufa kabla hujapata vile ulivyoweka kama lengo kuu.

 

Lengo kuu la Maisha yako liwe ni kusudi la wewe kuwepo hapa duniani. Ukianza kujua hilo na ukalifanyia kazi utaondoka duniani ukiwa umeacha mabadiliko makubwa.

 

Hata kama tayari umeshapata vitu vyote ambavyo wengi huwa wanatamani kuwa navyo bado unaweza kuanza upya kulitimiza lengo kuu la Maisha yako.

 

Kwa kupitia group hili utaweza kugundua nini lengo kuu la Maisha yako hapa duniani. Utagundua kwamba Uliumbwa kwa kusudi lipi hasa na ufanyeje ili kufikia mafanikio kupitia hili group

Kwasababu hakuna mwenye majibu ni siku gani ataondoka dunianu au kesho yake itakwenda kuwaje kupitia hili group utaweza kuishi leo vizuri sana. Na ukiweza kuishi leo vizuri Maisha yako yatakuwa na furaha na utaweza kutimiza kusudi

Your Partner in Success

Anatory Clemence

Success Motivator, Teacher, Author & Entrepreneur

Phone: +255755267700

Email: anatoryclemence@gmail.com

Leave a comment